Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu wa vikosi vya MINUSTAH afariki dunia

Mkuu wa vikosi vya MINUSTAH afariki dunia

Mkuu wa vikosi vya Umoja wa Mataifa nchini Haiti, MINUSTAH, Jenerali José Luiz Jaborandy Jr. amefariki dunia.

Alikuwa na umri wa miaka 57 na amehudumu kwenye nafasi hiyo kuanzia Machi 2014 alipoteuliwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon.

Akihojiwa na Radio ya Umoja wa Mataifa,Mkuu wa mawasiliano ya kijeshi wa MINUSTAH, Kanali Pedro Gagliardi amesema Jenerali Jaborandy Jr. raia wa Brazil, amefariki dunia akiwa kwenye ndege akitokea Marekani kuelekea Brazil.

(sauti ya Kanali Pedro)

“Jenerali alikuwa ni kiongozi mzuri sana, ameweza kutuongoza kwa urahisi mno, alikuwa ni askari mwenye ari na hekima sana, na tunasikitishwa sana na kifo chake, na tutamkumbuka daima. Na tutamkumbuka kwa sisi,walinda amani kusimama imara daima na kuzingatia dhamira yetu, na tutaendelea na kazi yetu vizuri, kama heshima ya kumbukumbu yake.”