Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maspika wanawake wataka kasi ya usawa wa kijinsia

Maspika wanawake wataka kasi ya usawa wa kijinsia

Awali kuelekea kuanza kwa mkutano huo wa nne, maspika wanawake wa  mabunge wametaka kuongezeka kwa usawa wa kijinsia kwa nguvu za pamoja, huku wakisisitiza umuhimu wa umoja katika fikra na matendo.

Katika majumuisho ya mkutano wa siku mbili mjini New York,  chini ya dhima ubunifu kwa ajili ya usawa wa kijinsia, maspika hao wamesema umoja huo ni chachu kubwa ya mabadiliko katika kufanikisha usawa katika kizazi kimoja.

Taarifa ya majumuisho inaongeza kuwa mabadiliko ya haraka yanawezekana kwa changamoto na kubadilisha mitizamo ambayo inaendeleza tabia, tamaduni na imani ambazo zinasababisha ukosefu wa usawa.

Wamesema kuwa licha ya mawasiliano madhubuti katika masuala ya usawa wa kijinisia, na kufanya kazi kwa karibu na jamii, elimu juu ya usawa wa kijinsia kwa wasichana na wavulana ni jambo la kipaumbele.

Kadhalika umuhimu wa vijana kuwatizama wanawake na wanaume kama viongozi na mfano umesisitizwa na kundi la viongozi hao .