Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la usalama lapongeza makataba wa amani Sudan Kusini

Baraza la usalama lapongeza makataba wa amani Sudan Kusini

Baraza la usalama limekaribisha utiliwaji saini wa makataba wa amani mnamo Agosti 26 uliotekelezwa na Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir Mayardit , kiongozi wa upinzani Dk Reik Machar Teny pamoja na mwakilishi wa wafungwa Pagan Amum Okiech mnamo Agosti 17 na wadau wengine.

Katika taarifa yake wajumbe wa baraza la usalama wameelezea kusikitishwa kwao ikiwa upande wowote hautawajibika vyema katika utekelezaji mkataba huo huku ikipongeza kwa dhati kazi iliyofanywa na jumuiya ya kimataifa ya IGAD katika kuongoza mchakato huo tangu kuanza kwa mgogoro hadi walipopanua wigo kwa kuhusisha Umoja wa Mataifa , na marafiki wa Sudan Kusini ili kufikia amani nchini humo.

Baraza la ualama limetambua kuwa makubaliano hayo ni hatua ya kwanza katika kupunguza madhila ya kisiasa na kiuchumi, kibinadamu na kiusalama yaliyotokana na machafuko nchini Sudan Kusini na kutaka jumuiya kimataifa kuunga mkono juhudi za kutekeleza makubaliano hayo.

Kadhalika baraza limetaka pande kinzani hima kusitisha mapigano ikiwa ni uthibitisho wa wa kukubali mamlaka ya Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo UNMISS kusaidia utekelezaji wa majukumu muhimu katika makubaliano.