Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Upatikanaji wa maji Afrika Mashariki

Upatikanaji wa maji Afrika Mashariki

Maji ni uhai! Huu ni usemi uliozoeleka sana katika masikio ya wengi.Pamoja na ukweli usiopingika katika usemi huu, bado upatikanaji wa maji hususani katika nchi zinazoendelea ni kitendawili.Wakati wiki ya maji imeanza ulimwenguni kuanzia Agosti 23 hadi 28 huko Stockholm Sweden inaelezwa kuwa hatua muhimu zimepigwa katika miaka kumi na mitano iliyopita.

Kaulimbiu ya maadhimisho haya ya miaka 25 ni “maji kwa ajili ya maendeleo” Ripoti zinasema kwamba takriban watu bilioni mbili watakosa huduma ya maji salama na karibu watu bilioni 2.5 watakosa huduma za kujisafi. Zaidi ya watu bilioni moja watakuwa hawana huduma ya nishati umeme na takriban watu bilioni moja wata lala na njaa, idadi kubwa yao ikiwa ni watu masikini.

Maji ni muhimu katika kukabiliana na changamoto hizi kwani maisha yetu na viumbe vingine wanategemea maji kwa uhai. Bila maji hakuwezi kuwa na uchumi endelevu na kuishi maisha bora na kuzalisha chakula, nishati na mahitaji muhimu. Ni kwa mantiki hiyo ambapo wiki ya maji duniani mjini Stockholm inaangazia maswala haya. Je hali ikoje Afrika Mashariki? Tuanzie Uganda ambapo John Kibego anaangazia uaptaikanaji wa maji nchini humo.

(PACKAGE KIBEGO)

Na sasa tuelekee nchini Tanzania kwake Hamis Makungu wa redio washririka Pangani Fm ya Tanga .

(PACKAGE HAMIS)

Nakutakieni wikendi njema.