Idadi ya wakibizi na wahamiaji wanaosaka hifadhi Ulaya yazidi kuongezeka

28 Agosti 2015

Idadi ya wakimbizi na wahamiaji wanaovuka bahari ya Mediterranean mwaka huu sasa imevuka 300,000 ikiwamo kiasi cha 200,000 wanaowasili Ugiriki na wengine 110,000 nchini Italia, limesema shirika la Umoja wa Matafa la kuhudumai wakimbizi UNHCR ambapo limebainisha kuwa mwaka jana watu 219,000 ndio waliovuka bahari hiyo kusaka hifadhi.

Kwa mujibu wa UNHCR wakimbizi 2,500 wamekufa au kupotea mwaka huu wakati wakijaribu kueleeka Ulaya, idaid hii ikiwa haijumuishi tukio la wakimbizi waliokufa hapo jana nchini Libya.

Mwaka jana watu3,5000 walifariki au kupotea wakati wanavuka bahari ya Mediterranean ikiwa ni juhudi za kusaka hifadhi.

Katika siku za hivi karibuni watu wengi wameripotiwa kufariki katika matukio tofauti ambapo katika pwani ya Libya kikosi cha uokozi kilifanya operesheni . Boti mbili zilizokuwa zimebeba wahamiaji na wakimbizi 500 walikamatwa ambapo watu 200 wanasadikiwa kufa.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter