UM Tanzania wafanya usafi sokoni kuadhimisha miaka 70 ya UM

28 Agosti 2015

Umoja wa Mataifa nchini Tanzania uanaendelea na shughuli mbalimbali za kijamii katika kuadhimisha miaka 70 ya Umoja huo.

Wakiambatana na maafisa mbalimbali wa serikali na wananchi maafisa kadhaa wamefanya usafi katika soko la Temeke mjini Dar es salaam ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha kutunza mazingira.

Mkurugenzi wa idara ya ushirikiano wa kitaifa wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa wa Tanzanai, Balozi Celestine Mushy anazungumzia umuhimu wa kutunza mazingira.

(SAUTI)

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter