Sudan ipindue hukumu ya kumchapa msichana wa shule- Wataalam wa UM

28 Agosti 2015

Wataalam wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa, wameeleza kusikitishwa na hukumu iliyotolewa nchini Sudan dhidi ya msichana wa shule aitwaye Ferdous Al Toum, ya kuchapwa viboko 20 hadharani na kulipa faini kwa kosa lililotajwa kama ‘kuvaa vazi lisiloonyesha heshima’.

Hii inafuatia msichana mwingine wa shule aitwaye Rehab Omer, kupewa faini kubwa kwa kosa kama hilo.

Wataalam hao wamesema kupigwa kwa wanawake hadharani ni desturi inayoendelea nchini Sudan, na kwamba kosa la ‘kutoonyesha heshima’ na adhabu ya kipigo hutumiwa kuwaadhibu wanawake kwa njia isiyo ya usawa.

Wataalam hao wametoa wito hukumu hiyo ipinduliwe, na wasichana waliozuiliwa kuachiwa huru mara moja. Aidha, wametoa wito kwa serikali ya Sudan ifanyie marekebisho sheria inayowabagua wanawake kwa misingi ya jinsia yao na kutimiza viwango vya kimataifa.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter