Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban kuzuru Uchina 2 – 6 Septemba, 2015

Ban kuzuru Uchina 2 – 6 Septemba, 2015

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, atafanya ziara nchini Uchina kuanzia Septemba 2 hadi 6.

Katibu Mkuu amealikwa na rais wa Uchina Xi Jinping kuhudhuria hafla ya kumbukizi mjini Beijing, katika kuadhimisha miaka 70 tangu kumalizika vita vikuu vya pili vya dunia.

Akiwa Beijing, Bwana Ban amepanga kukutana na Rais Xi; Waziri Mkuu wa Baraza la Kitaifa la Uchina,  Li Keqiang; Makamu wa Rais Liu Yandong, na Waziri wa Mambo ya Nje,  Wang Yi. Miongoni mwa mambo wanayotarajiwa kujadili ni masuala maadhimisho ya miaka 70 ya kuanzishwa Umoja wa Mataifa, mabadiliko ya tabianchi na mkutano ujao wa maendeleo endelevu.