Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNESCO yalaani mauaji ya mwandishi wa televisheni Somalia

UNESCO yalaani mauaji ya mwandishi wa televisheni Somalia

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu , Sayansi na Utamaduni(UNESCO), Irina Bokova amelaani mauaji ya mwandishi wa habari wa Somalia Abdikarim Moallim Adam, ambaye alikuwa ripoti wa kituo cha televisheni kiitwacho Universal.

Taarifa ya UNESCO inamnukuu Bi Bokova akisema kuwa waandishi wa Somalia wanalipa kile alichokiita garama isyokubalika, katika kuendelea kuhabarisha nchi yao na dunia nzima.

Amesema kuwa usalama wa wanataaluma hao una muhimu mkubwa kwa wote wanaotaka kuona machafuko yanakomeshwa kwa njia ya majadiliano na maelewano.

Mwanahabari huyo aliyeuwawa alikuwa nje ya hotel Jazeera Palace mjini Mogadishu mnamo Julai 26 wakati gari lilipolipuka kwa bomu na kusababisa mauti yake.