Baraza la Usalama lakutana kujadili hali ya kibinadamu Syria

Baraza la Usalama lakutana kujadili hali ya kibinadamu Syria

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, limekuwa na mkutano leo kuhusu hali kya kibinadamu nchini Syria, ambako zaidi ya watu robo milioni wameuawa, na zaidi ya watu milioni moja kujeruhiwa, tangu mzozo ulipoanza nchini humo.

Akihutubu katika kikao hicho, Mratibu wa masuala ya kibinadamu, Stephen O’Brien, amesema wakimbizi wa Syria zaidi ya milioni nne, wamevuka mpaka kutafuta usalama katika nchi jirani na kwingineko, huku zaidi ya watu milioni 7.6 wakilazimika kuhama makwao ndani ya nchi.

Bwana O’Brien amesema idadi kubwa ya wakimbizi kutoka Syria inatoa shinikizo kubwa kwa nchi zinazowahifadhi na jamii za wenyeji wao, na hivyo kutoa wito...

(SAUTI OBRIEN)