Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Djokovic ateuliwa balozi mwema wa UNICEF #NovakforChildren

Djokovic ateuliwa balozi mwema wa UNICEF #NovakforChildren

Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya watoto, UNICEF, leo limetangaza kuteuliwa kwa nyota mchezo wa tennis, Novak Djokovic kuwa Balozi wake Mwema.

Djokovic, ambaye ndiye mcheza tennis nambari moja duniani, amekuwa akimulika masuala ya watoto walio hatarini na jamii zao kupitia nafasi yake kama Balozi wa UNICEF nchini Serbia na kupitia wakfu wake wa Novak Djokovic Foundation.

Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa UNICEF, Yoka Brandt, amempongeza Djokovic kwa uteuzi huo mpya kwenye makao makuu ya UNICEF  mjini New York, katika hafla iliyomjumuisha pia rais wa Benki ya Dunia, Dr. Jim Yong Kim .

Bi Brandt amesema Novak Djokovic ni bingwa wa kweli wa watoto kote duniani, na kwamba ameonyesha kuwa sauti yenye nguvu na vitendo mathubuti vinaweza kuleta mabadiliko kwa maisha ya watoto wakiwa wangali wadogo sana.