Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Rais Kiir wa Sudan Kusini asaini mkataba wa amani

Rais Kiir wa Sudan Kusini asaini mkataba wa amani

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir amesaini makubaliano ya amani ambayo huenda yakamaliza mgogoro wa Sudan Kusini yaliyodumu kwa takrini miaka miwili.

Katika hafla fupi ya utiaji saini huo, Rasi Kiir amesema lazima demokraia ya nchi hiyo iheshimiwe lakini akatoa onyo..

(SAUTI KIIR)

‘‘Uongozi wa kisiasa na serikali iliyochaguliwa kidemokrasia isipuuzwe. Kwahiyo tunasaini mkataba huu , lakini nawaonya ninyi viongozi wa kanda kusimama nasi katika utekelezaji’’.

Awali msemaji wa Rais Kiir Ateny wek Ateny amesema kiongozi huyo ana dhamira ya kweli na kuongeza kuwa kipaumbele cha serikali ijayo ni kupata amani na upatanisho .