Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Akiwa Paris, Ban awahutubia mabalozi wa Ufaransa kuhusu mabadiliko ya tabianchi

Akiwa Paris, Ban awahutubia mabalozi wa Ufaransa kuhusu mabadiliko ya tabianchi

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, ambaye yupo ziarani nchini Ufaransa, leo amehutubia mkutano wa mabalozi wa Ufaransa kuhusu suala la mabadiliko ya tabianchi.

Ban amewashukuru mabalozi hao kwa uungaji mkono kazi ya Umoja wa Mataifa kwa muda mrefu, akisema Ufaransa ni ya nne katika kuchangia kwa kiasi kikubwa bajeti ya ujumla ya Umoja wa Mataifa, na ya tatu kuchangia bajeti ya operesheni za ulinzi wa amani.Akizungumza kuhusu kongamano la Paris kuhusu tabianchi mnamo Disemba mwaka huu, Bwana Ban amesema anatarajia kuwa kutakuwa matokeo yake yatakuwa hatua ya ujasiri na ya maana.