Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la usalama lakutana kujadili hali nchini Libya

Baraza la usalama lakutana kujadili hali nchini Libya

Baraza la usalama leo limekutana kujadili hali nchini Libya ambapo mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na mkuu wa ujumbe wa Umoja huo nchini Libya Bernardino León, amelihutubi abaraza hilo kwa njia ya video.Grace Kaneiya na taarifa zaidi.

(TAARIFA YA GRACE)

Nats

Wajumbe wa baraza wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa UNSMIL ambaye amelihutubia baraza hilo moja kwa moja kutoka Paris Ufaransa.

Bwana León, amesisitiza kuwa amani ya Walibya itapatikana kupitia Walibya wenyewe na jumuiya ya kimataifa ina jukumu la kusaidia tu huku akisema makubaliano ya amani yakifikiwa raia hao ndio washindi.

Amesema kuwa muda hautoshi na hivyo viongozi wa Libya waongeze msukumo katika majadiliano ambayo ameyaelezea kufikia hatua nzuri. Awali mkuu huyo wa UNSMIL ameelezea madhila wanayokumbana nayo raia wasio na hatia.

(SAUTI BERNADINO)

‘‘Kwa mujibu wa mashirika mbalimbali ya UM takribani  watu miloni moja nukta tisa waanahitaji  msaada wa haraka wa kibinadamu ili kupata mahitaji ya lazima ya afya . Upatikanaji wa chakula sasa ni tatizo kubwa kwa watu takribani milioni 1.2 wengi wao wakiwa Bengazi na Mashariki mwa nchi. Wakimbizi wa ndani Libya sasa wamefika laki nne. Huduma ya afya inaporomoka, hospitali nyingi zimezidiwa na hazina uwezo tena.’’

Bwana León pia amesema kundi la wanamgambo linatoka kuweka dola la kiisilamu Daesh limeendeeleza vitendo ambavyo ni kinyume na haki za binadamu huku uchumi wa Libya ukiendelea kuporomoka.