Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF yazindua mkakati wa kurejesha watoto shuleni Sudan Kusini

UNICEF yazindua mkakati wa kurejesha watoto shuleni Sudan Kusini

Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya watoto, UNICEF, limezindua kampeni ya kitaifa nchini Sudan Kusini ya kuongeza idadi ya watoto wanaoenda shule.

Mkakati huo uliong’oa nanga katika kata ya Pibor, unaotoa fursa ya kupata elimu kwa watoto, barubaru na walioacha shule kwa sababu za umaskini, ubaguzi wa kijinsia au mgogoro.

Kama sehemu ya uzinduzi huo, shule kadhaa na miundombinu mingine iliyojengwa kwa usaidizi wa USAID na Muungano wa Ulaya, EU, zilikabidhiwa kwa mamlaka za eneo la Pibor.

Stefano Del Leo ni mkuu wa ujumbe wa EU mjini Juba..

(Sauti ya Stefano Del Leo)