Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban amteua Koen Davidse wa Uholanzi kuwa Mwakilishi wake maalum Mali

Ban amteua Koen Davidse wa Uholanzi kuwa Mwakilishi wake maalum Mali

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, ametangaza leo kuteuliwa kwa Koen Davidse wa Uholanzi kuwa Naibu Mwakilishi wake maalum katika Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Mali, MINUSMA.

Bwana Davidse  atamrithi Bwana Arnauld Akodjènou wa Benin, ambaye muda wake wa kuhudumu kama Naibu Mwakilishi Maalum mnamo mwezi Septemba.

Katibu Mkuu ametoa shukrani zake kwa Akodjènou’s kwa huduma yake ya kujitoa nchini Mali katika mazingira magumu.

Bwana Davidse ana uzoefu wa miaka 25 ya huduma kwenye ngazi ya kimataifa, akiwa amehudumu katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Uholanzi, kwenye Benki ya Dunia na katika Umoja wa Mataifa.