Skip to main content

UNHCR yahaha kunusuru maelfu ya wanaomiminika Ugiriki.

UNHCR yahaha kunusuru maelfu ya wanaomiminika Ugiriki.

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), linashirikiana na mamlaka za serikali ya Serbia kutoa  huduma za kibinadamu kwa maelfu ya wasaka hifadhi na wakimbizi   kwenye mpaka wa Ugiriki na iliyokuwa jamhuri ya Yugoslavya Macedonia. Taarifa kamili na Amina Hassan

(Taarifa ya Amina)

Wakati idadi ya wakimbizi wanaongia nchini Ugiriki inatarajiwa kufika zaidi ya 3,000 kila siku, UNHCR na serikali ya Serbia wanapambana kufikia mahitaji ya wakimbizi zaidi ya 10,000 walioingia nchini humo hivi karibuni, wengi wakitoroka nchi zenye migogoro kama Syria na Afghanistan.

Licha ya uwepo wa hali ya utulivu, UNHCR imeguswa na hali ya wakimbizi hao na kubaini uhutaji kushirikiana na kushughulikia wakimbizi kwa moyo wa utu. Melissa Fleming ni msemaji wa UNHCR mjini Geneva

(Sauti Fleming)

“Hua ni wachovu kimwili na wakikumbwa na kiwewe, wakihitaji dawa na msaada wa kibinadamu hususani vikundi vilivyo hatarini zaidi kama wagonjwa, wajawazito na wazee. Ni muhimu kuwashughulikia kwa ubinadamu na kuhakiskisha kwamba wamepata mahitaji muhimu. Yanajumwisha uitikio wa mahitaji yao ya msingi na kuheshimu haki za wakimbizi, wanaosaka hifadhi na wahamiaji”