Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tumesikitishwa na kifungo cha Rais mstaafu Maldives; Kamishna Zeid

Tumesikitishwa na kifungo cha Rais mstaafu Maldives; Kamishna Zeid

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu Zeid Ra'ad Al Hussein, ameelezea kusikitishwa kwake kufuatia hatua ya serikali ya Maldives kumrejesha tena kifungoni Raisi mstaafu wa nchi hiyo Mohammad Nasheed siku ya Jumapili. Joseph Msami na maelezo kamili

(TAARIFA YA MSAMI)

Kamishana Zeid amenukuliwa leo mjini Geneva akiwaambia waaandishi wa habari kuwa Umoja wa Mataifa awali ulifaraijika na taarifa kuwa amechiliwa kutoka kizuizini baada ya jamii ya kitaifa na kmataifa kukosoa kifungo kisicho halali cha miaka 13 dhidi ya kiongozi huyo mnamo mwezi Machi.

Amesema kuwa nguvu kupita kiasi ikiwamo maji ya mwasho vilitumika dhidi ya wanaomuunga mkono ambao walikusanyika katika makazi yake ili kuonyesha mshikamano na kupinga kurejeshwa tena kifungoni. Rupert Colville ni msemaji wa ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa

(SAUTI)

‘‘Ofisi ya haki za binadamu ilipeleka ujumbe mara mbili nchini Maldives katika miezi ya hivi karibuni,  kujadili masuala haya na mamlaka. Pia ilimtembelea Bwana Nasheed  jela na nyumbani kwake ambako alizuiliwa. Kurejeshwa jela kwa Nasheed kwa mtizamo wetu kunarudisha nyuma hali ya haki za binadamu pamoja na juhudi za kupatiakana kwa suluhu la kisiasa  nchini Maldives.’’