Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukibadili Nigeria, unabadili pia Afrika- Ban

Ukibadili Nigeria, unabadili pia Afrika- Ban

Wakati huohuo Katibu Mkuu Ban Ki-moon, amewaambia waandishi wa habari mjini Abuja kuwa anaamini kwamba Nigeria ikibadilika, bara Afrika pia litabadilika, akisifu uchaguzi wa Aprili mwaka huu, ambao ulihamishia mamlaka kwa upinzani kwa amani.

Ban amesema hayo muda mfupi baada ya kukutana na Rais Mohammadu Buhari, ambaye amesema amejadili naye mambo mengi, yakiwemo maendeleo, haki za binadamu na usalama, ikiwemo hali inayosikitisha ya viwango vya ukatili na ugaidi unaoenezwa na Boko Haram kaskazini mashariki mwa nchi na kwingineko.

Ban ameongeza nakariri mshikamano wangu wa dhati na watu wa Nigeria, serikali na familia za waathiriwa na waathiriwa wenyewe. Umoja wa Mataifa utafanya kazi nao kukabiliana na itikadi kali na ugaidi.

Aidha, Bwana Ban amezungumza kuhusu wasichana wa Chibok waliotekwa na Boko Haram, ikiwa ni siku 500 wiki hiii tangu kutekwa kwao akisema kuwa kitendo hicho kamwe hakikubaliki.

Kadhalika amesema kwamba anataka kukariri mshikamano wangu na wasichana wa Chibok, na wasichana wengine wengi wasio na hatia na wavulana, ambao majina na hatma yao bado haijulikani. Haikubaliki kuwa maisha yao na elimu yao imevurugwa hivi. Dunia nzima imeguswa na hatma yao.

Bwana Ban ametoa wito kwa waliowateka wasichana hao na watoto wengine wengi wawaachie huru bila masharti