Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mfumo wa kukusanya taarifa za maji utawezesha kuimarisha mazao: FAO

Mfumo wa kukusanya taarifa za maji utawezesha kuimarisha mazao: FAO

Shirika la chakula na kilimo duniani, FAO limeanizisha mradi wa kukusanya taarifa za maji kwa ajili ya kusaidia nchi zilizoko karibu Afrika mashariki na kaskazini kuweza kusimamia vyema raslimali hii adhimu.

Mradi huo wa FAO umezinduliwa katika kongamano la wiki ya maji duniani, inayoadhimishwa Agosti 23 hadi 28, mjini Stockholm Sweden.

Kulingana na FAO mfumo huo wa setelaiti unalenga kukusanya  na kuchunguza taarifa ambazo zinaweza kutumika kuimarisha uzalishaji wa ardhini maji, na kuimarisha mifumo ya kilimo. Aidha, taarifa hizo zitakuwa wazi kwa kila nchi ambayo inazihitaji.

Shirika hilo linasema kwamba nchi zote zilizoko katika Afrika kaskazini na karibu na mashariki zinakabiliwa na uhaba wa maji, hali ambayo inaathiri kilimo ambako maji mengi hutumika.

Kadhalika FAO inasema kwamba uhaba wa maji huathiri usalama wa chakula na juhudi za  kumaliza umasikini, hususan katika maeneo ya vijijini ambako maji hutegemewa kwa viwango vya juu kwa ajili ya uzalishaji wa kilimo na mifugo.

Aidha upatikanaji wa maji ni muhimu kama upatikanaji wa huduma ya afya na elimu katika maeneo hayo.