Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tulizembea kudhibiti Ebola sasa hakuna kulala: WHO

Tulizembea kudhibiti Ebola sasa hakuna kulala: WHO

Mkurugenzi Mkuu wa shirika la afya ulimwenguni WHO Dr Margaret Chan amekiri kuwa jamii ya kimataifa ilichelewa kuchukua hatua katika kudhibiti homa kali ya Ebola iliyozikumba nchi za Afrika Magharibi takrbani miezi sita iliyopita.

Akihutubia kamati ya viwango wastani vya udhibiti wa afya kimataifa mjini Geneva kuhusu jumuku la chombo hicho katika kudhibiti Ebola, Dk Chan amesema WHO na wadau wa afya walichelewa kufahamu madhara ya mlipuko huo na akasem cha kufanya sasa ni.

(SAUTI DK CHAN)

‘‘Jukumu letu sasa ni kuangalia maboresho ambayo yataifanya dunia ijiandae vyema kwa mlipuko mwingine usioepukika, kwani kudhibiti kuenea kwa ugonjwa ni muhimu na ni jukumu la kihistoria la WHO".

Mkuu huyo wa WHO amesema pia kuwa licha ya shirika hilo kudhibiti mara 22 milipuko ya Ebola , kiliochotokea Afrika Magharibi kilisabibisha athari kubwa za kiuchumi akiangazia kuzuiwa kwa safari za ndege katika nchi hizo.

(SAUTI DK CHAN)

"Hatua hizi zilizitenga zaidi nchi hizi tatu na kuongeza machungu ya kiuchumi kwa watu maskini zaidi duniani."