UM walaani mashambulizi dhidi ya wahudumu wa kibinadamu CAR

24 Agosti 2015

Mratibu wa masuala ya kibinadamu katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, Aurélien Agbénonci, amelaani vikali  mashambulizi dhidi ya wafanyakazi wa kibinadamu yaliyotokea hivi karibuni katika mji wa Bambari na kujeruhi mfanyakazi mmoja wa Shirika la Msalaba mwekundu. Taarifa kamili na John Kibego

(Taarifa ya John Kibego)

Mashambulizi hayo yametokana na mapigano mapya baina ya  vikundi mbali mbali na kusababisha vifo vya raia angalau watano na kujewaruhi wanane.

Akilaani mashambulizi hayo, Bwana Agbénonci ametoa wito kwa wanaozozana kuwalinda wafanyakazi wa kibinadamu wanaotoa misaada kwa maelfu ya watu walioathirika na mgogoro. Amesema pia hali ya ubinadamu nchini humo ni ya kutisha na kanuni za kutopendelea upande wowote, uhuru na uadilifu na kanuni za sheria ya kimataifa ya kibinadamu ni lazima ziheshimiwe.

Tangu kuanza kwa mgogoro wa CAR, wafanyakazi 19 wa masuala ya kibinadamu wamepoteza maisha yao.

Mratibu huyo ametoa wito kwa pande zote kuhakikisha kwamba wanaotoa misaada ya kibinadamu wanaendesha shughuli zao bila kizuizi na kwa usalama, ili kuwafikia watu wenye mahitaji.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter