Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban asihi utulivu na mazungumzo ya amani kwenye rasi ya Korea

Ban asihi utulivu na mazungumzo ya amani kwenye rasi ya Korea

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amekaribisha mkutano wa ngazi ya juu kati ya Jamhuri ya Watu wa Korea, DPRK na Jamhuri ya Korea, ambao umefanyika hapo jana Jumamosi.

Bwana Ban amezingatia pia makubaliano kuwa mazungumzo yatarejelewa leo.

Katibu Mkuu amezihimiza pande zote kutumia mazungumzo hayo kurejesha utulivu na kuendeleza amani na ustawi kwenye rasi ya Korea.

Aidha, Bwana Ban ametoa wito kwa pande hizo kuongeza juhudi zao maradufu ili kutatua tofauti zao kupitia mazungumzo, huku zikijiepusha na vitendo vinavyoweza kuharibu mazingira ya mazungumzo.