UM walaani mauaji ya wanawake wagombea ubunge Mosul, Iraq

UM walaani mauaji ya wanawake wagombea ubunge Mosul, Iraq

Kaimu Mkuu wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq, UNAMI, na Naibu Mwakilishi wa Katibu Mkuu nchini humo, Gyorgy Busztin, amelaani vikali kuuawa kwa wanawake watatu wagombea viti vya ubunge katika mji wa Mosul.

Bwana Busztin ameeleza kukasirishwa na mauaji hayo yaliyodaiwa kufanywa na kundi linalotaka kuweka dola la Uislamu wenye itikadi kali, ISIL, akisema si ya kwanza kufanyika dhidi ya wagombea viti vya ubunge.

Akituma risala za rambirambi kwa familia za wahanga, Mjumbe huyo wa Umoja wa Mataifa ametoa wito kwa serikali ya Iraq kufanya kila iwezalo kuwafikisha waliotenda uhalifu huo mbele ya sheria.