Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tamasha la kuwaenzi watoa misaada ya kibinadamu lapambwa na burudani

Tamasha la kuwaenzi watoa misaada ya kibinadamu lapambwa na burudani

Wiki hii dunia imeadhimisha siku ya kimataifa ya misaada ya kibinadamu, na katika kuenzi siku hii hapa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa limefanyika tamasha maalum ili kuwaenzi wale waliopoteza maisha wakiwa katika harakati za kutoa misaada ya kibinadamu.

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya kibinadamu OCHA waliratibu tamasha hilo lililosheheni burudani mbalimbali. Ungana na Joseph Msami katika makala inayokupeleka katika eneo la tukio.