Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu wa UNESCO alaani mauaji ya mwandishi habari Sudan Kusini

Mkuu wa UNESCO alaani mauaji ya mwandishi habari Sudan Kusini

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Matifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO, Irina Bokova, ametoa wito uchunguzi ufanyike kuhusu mauaji ya mwandishi wa habari wa gazeti Peter Moi Julius yaliyotokea mjini Juba mnamo Agosti 19.

Bi. Bokova amelaani mauaji hayo akisema kwamba raia wanategemea vyombo vya habari ili kuweza kufanya maamuzi bora na kwa hiyo ni lazima waandishi habari waruhusiwe kufanya kazi katika mazingira salama.

Kwa mantiki hiyo ametoa wito kwa mamlaka kufanya uchunguzi kwa ajili ya kuwezesha haki za waandishi habari na kuzingatia sheria.

Marehemu Peter Julius Moi alikuwa anafanya kazi na gazeti la New Nation mjini Juba. Alipigwa risasi wakati akielekea nyumbani kutoka kazini.