Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yatiwa wasiwasi na hali kwenye mpaka wa Ugiriki na Macedonia

UNHCR yatiwa wasiwasi na hali kwenye mpaka wa Ugiriki na Macedonia

Shirika la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR, limeeleza kutiwa wasiwasi na hali inayozidi kuwa tete kwenye mpaka wa Ugiriki na Macedonia ilokuwa Jamhuri ya Yugoslavia (FYROM), ambako nguvu zilitumiwa kuwazuia watu kuvuka mpaka.

UNHCR imetiwa wasiwasi hasa kuhusu maelfu ya wakimbizi na wahamiaji, hususan wanawake na watoto, ambao sasa wamerundikana mpakani upande wa Ugiriki, kwenye mazingira yanayozidi kudidimia.

Kamishna Mkuu wa UNHCR, António Guterres amezungumza leo na Waziri wa Mambo ya Nje wa FYROM spoke today with FYROM Nikola Poposki kuhusu hali hiyo, ambaye amemhakikishia kuwa moaka hautafungwa siku zijazo.

Huku ikielewa shinikizo linaloikabili FYROM na wasiwasi  kuhusu usalama, UNHCR inatoa wito kwa serikali iweke utaratibu unaohitajika ili kuweka mfumo wa kudhibiti mpiaka ulio taratibu na unaojali ulinzi wa watu. Imetoa wito pia kwa serikali ya Ugiriki kuimarisha mipango ya kupokea na kuwasajili watu wanaohitaji ulinzi wa kimataifa, ili kuwasaidia watu walioko upande wa Ugiriki waende kwenye vituo vya mapokezi ya wakimbizi mbali na mpaka.