Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vijana wakutana Sweden kujadili mabadiliko ya tabianchi

Vijana wakutana Sweden kujadili mabadiliko ya tabianchi

Mkutano wa kimataifa wa vijana unaojadili mikakati ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi umeanza hapo jana nchini Sweden, ukilenga kukusanya maazimio ili kuyawasilisha katika mkutano wa mabadiliko ya tabia mjini Paris Ufaransa COP 21.

Mwakilishi wa Tanzania katika mkutano huo Rahim Nasser kutoka mtandao wa vijana wa mabadiliko ya tabia nchi CAN amemweleza Stella Vuzo wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa nchini humo namna vijana wanavyochangia uharibifu wa mazingira.

(SAUTI RAHIM)

Mkutano huo utadumu kwa siku kumi hadi Agosti 30 .