Ban atoa wito kwa Rais Nkurunziza kujikita kwa ujumuishaji na maridhiano

20 Agosti 2015

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amezingatia kuapishwa kwa Pierre Nkurunziza kama rais wa Burundi kwa muhula wa tatu, mjini Bujumbura.

Bwana Ban amekariri wito wake kwa wadau wote Burundi kufanya mazungumzo ya wazi na jumuishi ya kisiasa, chini ya Rais Yoweri Museveni, ambaye ni mpatanishi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, EAC.

Aidha, Ban amesema kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa kama ilivyowekwa katika andiko la EAC la Julai 6, kunahitaji kutokana na mazungumzo ya kuaminika nay a wazi, ili kuondoa migawanyo mikubwa iliyopo kisiasa.

Katibu Mkuu ametoa wito kwa Rais Nkurunziza kuandama barabara ya ujumuishaji na maridhiano.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter