Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama lamulika marekebisho katika sekta ya usalama

Baraza la Usalama lamulika marekebisho katika sekta ya usalama

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, leo limekutana kujadili uimarishaji wa amani na usalama wa kimataifa, likimulika hasa marekebisho ya sekta ya usalama. Taarifa kamili na Amina Hassan.

(Taarifa ya Amina)

Katika kikao cha leo, Baraza la Usalama limesikiliza hotuba za Bwana Dmitry Titov, Msaidizi wa Katibu Mkuu kuhusu utawala wa sheria na taasisi za usalama katika Idara ya Operesheni za Ulinzi wa Amani, Bi Izumi Nakamitsu, Msaidizi wa Mkuu wa Shirika la Mpango wa Maendeleo, UNDP, na Bi Zainab Hawa Bangura, Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu kuhusu ukatili wa kingono katika migogoro.

Katika hotuba yake, Bi Bangura amesema kukabiliana na ukatili wa kingono katika migogoro kwa njia ya kina kunahitaji ushirikiano wa karibu na sekta ya usalama, akipendekeza hatua nne zinazopaswa kuchukuliwa ili kukabiliana na tatizo la ukatili wa kingono katika vita. Kwanza ni kujumuisha suala la ukatili wa kingono katika marekebisho ya sekta ya usalama, pili uwajibishaji wa wahalifu, tatu, mafunzo ya kuwezesha kuzuia ukatili wa kingono.

Na nne, tuhakikishe usawa wa uwakilishi wa wanawake katika sekta za usalama kwa ngazi zote, ili kuwa na vikosi vya usalama vinavyoheshimu na kuwalinda wanawake na watoto, wakati wa vita na amani.”