Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hakuna maendeleo endelevu bila kuzingatia mabadiliko ya tabianchi: Pasztor

Hakuna maendeleo endelevu bila kuzingatia mabadiliko ya tabianchi: Pasztor

Msaidizi wa Katibu Mkuu kuhusu mabadiliko ya tabia nchi Janos Pasztor amesema agenda ya maendeleo endelevu haiwezi kutekelezwa ipasavyo ikiwa mabadiliko ya tabia nchi hayatapewa kipaumbele. Grace Kaneiya  na malezo kamili.

(TAARIFA YA GRACE)

Katika mahojiano na redio ya Umoja wa Mataifa Bwana Pasztor ameelezea kufurahishwa kwake na hatua ya nchi wanachama kutia saini ajenda ya maendeleo endelevu,  akisema kuwa ajenda hiyo inategemea kwa asilimia kubwa hatua za makabiliano dhidi ya  mabadiliko ya tabianchi.

Bwana Pasztor amesema ajenda hiyo ni muhimu na inazingatia mabadiliko ya tabianchi kwa kuwa.

(SAUTI PASZTOR)

‘‘Inahusu nishati endelevu, kujenga miji bora, kufanikisha usalama wa chakula, elimu, kuondoa umasikini na haya ndiyo mambo tunayohitaji kufanya ili kufanikisha mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabianchi.’’

Msaidizi huyo wa Katibu Mkuu kuhusu mabadiliko ya tabianchi amesema kuelekea katika mkutano wa mabadiliko ya  tabia nchi mjini Paris nchini Ufaransa mwezi Disemba, ana matumaini ya kufikiwa makubaliano yenye manufaa kwa kila nchi.