Skip to main content

Tanzania kuadhimisha miaka 70 ya UM kwa kutunza mazingira

Tanzania kuadhimisha miaka 70 ya UM kwa kutunza mazingira

Katika kuadhimisha miaka 70 ya Umoja wa Mataifa Tanzania imesema itaadhimisha siku hiyo kwa matukio kadhaa ya kutunza mazingira ikiwamo upandaji miti ikiwa ni sehemu ya kukabiliana  na mabadiliko ya tabianchi.

Katika mahojiano na afisa  habari wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania  Stella Vuzo

Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Celestine Mushy anafafanua .

(SAUTI BALOZI MUSHY)

Amesema tangu uwepo wa Umoja wa Mataifa Tanzania mwaka 1961, chombo hicho kimetoa mchango mkubwa katika ujenzi wa amani , na mendeleo katika sekta kama vile elimu na afya pamoja na kuondoa umasikini.