Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNRWA yatiwa hofu na kuzuka homa ya matumbo kwenye kambi ya Yarmouk, Syria

UNRWA yatiwa hofu na kuzuka homa ya matumbo kwenye kambi ya Yarmouk, Syria

Idadi ya watu walioambukizwa homa ya matumbo katika kambi ya Yarmouk mjini Damascus, imeongezeka karibu maradufu, kwa mujibu wa msemaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuwasaidia Wakimbizi wa Kipalestina, UNRWA, Chris Gunness.

Bwana Gunness amesema timu za UNRWA matibabu zilishuhudia visa sita hapo jana Jumanne katika wilaya ya Yalda, na visa vitano leo, na hivyo kufikisha idadi ya wagonjwa waliothibitishwa kuwa na homa ya matumbo kuwa kumi na mmoja.

Ameonya kuwa, kutokana na mazingira ya kambi ya Yarmouk, hali hiyo inatia wasiwasi, kwani UNRWA haijaweza kuifikia kambi hiyo iliyozingirwa tangu Machi 28, ilipotekwa na wapiganaji wa ISIS. Ametoa wito wahudumu wa kibinadamu wawezeshwe kufikia wakimbizi hao, kwani bila kufanya hivyo, raia wataendelea kuteseka.