Jumuiya ya kimataifa ihakikishe wanafunzi wa UNRWA wanarejea shuleni: UNESCO

19 Agosti 2015

Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la elimu sayansi na utamaduni UNESCO Irina Bokova ameelezea kusikitishwa kwake kufuatia ukosefu wa fedha uliosababisha kufungwa kwa shule za shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa Palestina UNRWA.

Katika barua yake kwa Kamishna Mkuu wa UNRWA Mr Pierre Krahenbühl., Bi Bokova amesema kuwa kwa watoto 500,000,  vigori pamoja na vijana 7,000 ambao wamekuwa wakipata mafunzo katika vituo vya UNRWA, elimu ni msingi wa kujenga mustakhabali mwema wa maisha yao.

Amesema ni jukumu la jumuiya ya kimataifa kuhakikisha fursa za kusoma kwa wote ili kuhakikisha wanafunzi wa UNRWA wanarejea shuleni kwa wakati.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter