Tunapaswa kuwasaidia wahitaji wa misaada ya kibinadamu: Kak'a

19 Agosti 2015

Tukisalia katika Siku ya Kimataifa ya misaada ya kibinadmau msakata kabumbu wa kimataifa wa Brazil Ricardo Kak'a ambaye ni miongoni mwa washiriki wa kampeni ya kuonyesha ubinadamu ameeleza umuhimu wa kampeni hiyo ili kuwafukia wahitaji wa misaada ya kibinadamu.

Katika mahojiano na redio ya Umoja wa Mataifa mwanamichezo huyo aliyewika na timu ya taifa ya Brazil na klabu ya Real Madrid kabla ya kuja kucheza soka hapa Marekani anaeleza namna alivyoshiriki.

(SAUTI Kak'a)

‘’Nimekuwa nikishiriki katika kampeni hii tangu ilipoanza, nilirikodi video mjini New York na nashirikisha mtandao wangu wa twita kusema mambo mengi hususani kuhusu Nepal ambako kuna usaidizi wa mahitaji ya kibinadamu kwa sasa. Kwahiyo kampeni hii ni muhimu na ni wakati wa kushirikisha watu kile tunachoweza kufanya kwa ajili ya wengine.’’

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter