WFP yawaenzi watoa huduma wa kibindamu
Kuelekea siku ya Kibinadamu Duniani, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP), Ertharin Cousin amewaenzi wahudumu wa kibinadamu wa mstari wa mbele. Taarifa kamili na John Kibego.
(Taarifa ya John Kibego)
Katika ujumbe wake kabla ya maadhimisho ya 12 ya mauaji ya wahudumu 22 wa shirika hilo katika shambulio la bomu kwenye ofisi ya Umoja wa Matifa mjini Baghdad, Cousin amesema shirika hilo linaomboleza vifo vya wenzao hao na kueleza kupoteza matumaini ya kupatikana kwa wenzao wengine 4 waliotoeka nchini Sudan mnamo mwaka uliyopita.
Amesema wakati wanaomboleza mauaji hayo, wanawapongeza wahudumu wa kibinadamu ambao sasa asilimia 80 wanahudumu katika mataifa na maeneo yenye migogoro.
Cousin amewahimiza wahudumu hao kufanya kazi bila hofu ingawa kufikia watu wanaohitaji misaada ya kibinadamu katika nchi kama Sudan Kusini na Yemen kunazidi kuwa kugumu.