Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNSMIL,OHCRC yalaani machafuko yanayotekelezwa na ISIL nchini Libya

UNSMIL,OHCRC yalaani machafuko yanayotekelezwa na ISIL nchini Libya

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Libya UNSMIL na ofisi ya haki za binadamu OHCHR wamelaani hatua ya wanamgambo wa kundi linalotaka dola la kiislamu ISIL kudai kukalia eneo liitwalo Sirte nchini Libya.

Taarifa zinasema kuwa UNSMIL imearifiwa na raia kuwa wengi wao wamekimbia eneo hilo ambalo lilishuudia mapigano makali mnamo Agosti 13  ambapo wilaya hiyo iliripotiwa kuiminiwa makombora na vikosi vya ISIL wakati wa mapigano.

Idaidi ya vifo kufuatia machafuko hayo haijajulikana rasmi lakini UNSMIL inakadiria kuwa kati ya watu wanne hadi 38 wameuwawa huku ISIL ikidaiwa kuteka nyara wanaume takribani 16 ambao usalama wao haujaulikani.

Rupert Colville ni msemaji wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya haki za bianadamu OHCHR

(SAUTI COLVILLE)

’Vikundi washirika wa ISIL pia wamekuwa wakiwashambulia watu kwa misingi ya dini zao, mathalani mwezi April mwaka huu ,kundi moja lilitoa video inayoonyesha mauji ya Wakristo 28 katika matukio mawili tofauti Libya.’’