Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vifo na uhalifu kuongezeka Syria: OHCHR

Vifo na uhalifu kuongezeka Syria: OHCHR

Siku chache baada ya shambulio katika soko nchini Syria , Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa OHCHR,  imesema vifo vitokanavyo na  mashambulizi ya silaha za kiholela huenda vikaongezeka na kuchochea  zaidi uhalifu wa kivita.Taarifa kamili na Joseph Msami.

(Taarifa ya Msami)

Shambulio hilo la angani linadaiwa kufanywa na vikosi vya serikali mjini Douma, Damascus na kusababaisha vifo vya zaidi ya watu 100 namajeruhi kadhaa.

Msemaji wa OHCRC Rupert Colville amewaambia waandishi wa habari mjini Geneva kuwa huenda idadi ya vifo kufuatia shambulio hilo ikaongezeka kutokana na  upungufu wa vifaa tiba kwa majeruhi ambao wanatibiwa katika hospitali ambazo haziko maeneo rasmi kufuatia miaka miwili ya kuzingirwa na vikosi.

Bwana Colville anaeleza kile manusura wa shambulio walichokisema

Kwa mujibu wa manusura, Jumapili kulikuwa na mashambulizi mawili, shambulizi la kwanza la anga kisha likafuatiwa na mashambulizi ya ardhi ambayo yaliwalenga watu waliokuwa wamewahi kuokoa waliouwawa na kujeruhuiwa na shambulio la anga.’’

Amesema kuwa raia huko Douma wameiambia Umoja wa Mataifa kuwa  hatua ya serikali kuzingira maeneo kumesababisha  vifo zaidi kuliko shambulizi la hivi karibuni japo lilikuwa la kutisha.