Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban ashutushwa na mlipuko Bangkok

Ban ashutushwa na mlipuko Bangkok

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban K-moon ameelzea kushtushwa kwake na taarifa za mlipuko mjini Bangkok nchini Thailand  katika eneo takatifu maarufu kwa  utalii liitwalo Erawan na kusababisha vifo vya raia wasio na hatia.

Bwana Ban ametuma salamu za rambirambi kufuatia mlipuko huo kwa familia athiriwa, watu na serikali ya Thailand, na kuwatakia uponyaji wa haraka majeruhi.

Bwana Ban ameelezea matumaini yake kuwa watekelezaji wa tukio hilo watafikishwa kwenye vyombo vya sheria.