Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban alaani mauaji ya Kanali Jean Bikomagu, Burundi

Ban alaani mauaji ya Kanali Jean Bikomagu, Burundi

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amelaani mauaji ya Kanali Jean Bikomagu, aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Burundi, ambayo yalitekelezwa na watu wasiojulikana mjini Bujumbura, mnamo Agosti 15.

Taarifa kutoka ofisi ya msemaji wake imesema kuwa Katibu Mkuu ametuma salamu za rambirambi kwa familia ya marehemu.

Aidha, Bwana Ban amelezwa kusikitishwa na mwelekeo wa machafuko ya kisiasa nchini Burundi, na kukaribisha uamuzi wa serikali kufanya uchunguzi, kuwakamata na kuwashtaki watu waliotenda mauaji ya hivi karibuni.

Katibu Mkuu amekariri wito wake kwa Warundi wote warejelee hima mazungumzo jumuishi na kutatua tofauti zao kwa amani, na kuahidi uungaji mkono wa Umoja wa Mataifa katika juhudi zinazolenga kujenga amani na ustawi Burundi.