Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban alaani shambulio la bomu Pakistan

Ban alaani shambulio la bomu Pakistan

Katibu  Mkuu wa Umoja wa Mataiaf Ban Ki-moon,  amelaani vikali shambulio la bomu hii leo jimboni Punjab nchini Pakistan,  lilosababaisha majeruhi na  vifovya watu kadhaa ikiwamo waziri wa mambo ya ndani wa nchi hiyo Shuja Khanzada.Grace Kaneiya na taarifa kamili.

(Taarifa Grace)

Taarifa ya msemaji wa Katibu Mkuu inamnukuu Bwana Ban akisisistiza kuwa hakuna kitu cha kuhalalisha ugaidi na kuelezea matumaini yake kuwa watekelezaji wa matukio hayo watafikishwa katika vyombo vya sheria.

Katibu Mkuu ametuma salamu zake za rambirambi kwa familia ,waathiriwa na kuwatakia uponyaji wa haraka majeruhi pamoja na kuelezea masikitiko yake kwa watu  na serikali ya Pakistan.