Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jumuiya ya kimataifa isitusahau: UNHCR Kenya

Jumuiya ya kimataifa isitusahau: UNHCR Kenya

Licha ya uwepo wa mahitaji ya dharura katika nchi kama vile Syria na Iraq, Shirika la Umoja wa Mataifa la wakimbizi UNHCR nchini Kenya limeitaka jumuiya ya kimataifa isisahau mahitaji makubwa ya kibinadamu ambayo yanawakabili wakimbizi walioko nchini humo.

Katika mahojiano na idhaa hii msemaji wa UNHCR Kenya Emmanuel Nyabera anasema wakimbizi walioko katika kambi za Kakuma na Daadab bado wanakabiliwa na upungufu wa mahitaji kama vile chakula na maji, na kuongeza kuwa idadi kubwa ya  wakimbizi inamiminika kutoka Sudan Kusini.

(SAUTI NYABERA)

Hata hivyo amesema licha ya uhaba huo,  juhudi za mashirika kama vile la chakula duniani WFP na mengineyo zimewezesha upatikanaji wa mahijtaji kama chakula na maji.