Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maswala ya watu wa jamii za asili yapaziwa sauti

Maswala ya watu wa jamii za asili yapaziwa sauti

Wiki hii Umoja wa Mataifa umeadhimisha siku ya kimataifa ya watu wa asili, ukiangazia swala zima la afya yao.

Nats…

Huyu ni Carlos Ponce Eagle Feather, yaani unyoya wa tai, kutoka jamii ya Wamaya, ambao wanaishi Amerika ya Kusini na ya Kati, akiimbia wimbo wa kiasili katika uzinduzi wa maadhimisho yaliyofanyika jumatatu hii, kwenye Umoja wa Mataifa mjini New York.

Akiongea wakati wa mkutano huo, Wu Hong-Bo, Mkuu wa Idara ya Maswala ya Kijamii na Kiuchumi wa Umoja wa Mataifa amesema mchango wa watu wa asili ni muhimu sana kwenye urithi wa dunia na kwa uendelevu wa maendeleo, lakini bado wanakumbwa na changamoto nyingi, hasa kwa upande wa afya.

(Makala)