Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ghasia na uhaba wa pesa yakwamisha misaada ya kibinadamu Mali

Ghasia na uhaba wa pesa yakwamisha misaada ya kibinadamu Mali

Mratibu wa Maswala ya Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa kwa ukanda wa Sahel, Toby Lanzer, ameonya kwamba uhaba wa chakula utazidi kuongezeka nchini Mali iwapo pande za mzozo watashindwa kuhakikisha utulivu nchini humo.

Ametoa wito kwa jamii ya kimataifa kuendelea kufadhili msaada wa kibinadamu nchini humo, hasa kwa watu wanaoteseka zaidi.

Kwa mujibu wa Ofisi ya kuratibu maswala ya kibinadamu OCHA, takriban watu milioni 3.1 nchini Mali bado wanakumbwa na ukosefu wa chakula, huku maisha ya watoto 15,000 yakiwa hatarini kwa sababu ya unyafuzi.

Kwa upande wake Mbaranga Gasarabwe, ambaye ni mratibu wa maswala ya kibinadamu nchini Mali, ameeleza kwamba ukosefu wa usalama unazuia usambazaji wa misaada ya kibinadamu kwenye baadhi ya maeneo ya nchi.

Halikadhalika, OCHA imeongeza kwamba asilimia 33 tu ya pesa zinazohitajika kwa ajili ya msaada wa kibinadamu zimefadhiliwa.