Skip to main content

UNHCR yahofia athari za machafuko kwa wakimbizi wa Nigeria

UNHCR yahofia athari za machafuko kwa wakimbizi wa Nigeria

Shirika la Kuhudumia Wakimbizi katika Umoja wa Mataifa, UNHCR, limeeleza kusikitishwa na kuongezeka kwa machafuko ndani na karibu na Nigeria na athari zake kwa hali ya wakimbizi wa Nigeria walioko katika nchi jirani.John Kibego na tarrifa kamili.

(Taarifa Kibego)

Aidha, shirika hilo limesema linasikitishwa na kupungua kwa fursa ya kibinadamu ya wakimbizi hao kuomba hifadhi.

UNHCR imepongeza ukarimu na moyo wa ubinadamu wa Cameroon, Chad na Niger kwa kufungua milango yao kwa makumi ya wakimbizi ambao wamekuwa wakikimbia machafuko nyumbani kwao kaskazini mashariki mwa Nigeria katika miaka miwili iliyopita.

Hata hivyo, UNHCR imesikitishwa na kurejeshwa nyumbani pasipo hiari kwa maelfu ya watu kutoka Cameroon na Chad mwezi Julai na Agosti.