Skip to main content

Usalama unazorota, tunahamisha wakimbizi Bujumbura: UNHCR

Usalama unazorota, tunahamisha wakimbizi Bujumbura: UNHCR

Kufuatia  vifo vya wakimbizi watatu mjini Bujumbura hivi karibuni shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR linatekeleza zoezi la kuhamishwa kwa wakimbizi katika kambi kwa ajili ya usalama.

Katika  mahojiano na idhaa hii Mwakilishi mkazi wa UNHCR nchini Burundi Abel Mbilinyi amesema vifo vya wakimbizi wawili majuma mawili yaliyopita na mkimbizi mwingine takribani mwezi uliopita ni miongoni mwa sababu za kuhamishwa kwa wakimbizi baada ya kufanya pia mashauriano na serikali.

(SAUTI MBILINYI)

Hata hivyo amesema zoezi hilo ni la hiari kwani sio maeneo yote ambayo yanakabiliwa na machafuko na kwamba mpaka sasa zaidi ya wakimbizi 1000 wameshahamishwa.