Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Saudia Arabia yatoa dola milioni 35 kwa Wapalestina

Saudia Arabia yatoa dola milioni 35 kwa Wapalestina

Ufalme wa Saudia umetangaza kutoa msaada wa dola milioni 35 kwa ajili ya kusaidia wakimbizi wa Palestina.

Kwenye taarifa yake, Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi wa Palestina UNRWA imesema kwamba pesa hizo zitasaidia kukarabati shule na vituo vya afya nchini Jordan, kujenga vituo vya afya vitatu kwenye Ukingo wa Magharibi na kusaidia huduma za afya na elimu kwenye Ukanda wa Gaza.

Aidha, dola milioni 19 kati ya pesa hizo zitachangia katika kupunguza ukata wa fedha unaolikumba shirika hilo.

Tangazo hilo linafuata ripoti iliyotolewa awali wiki hii na UNRWA ikisema kwamba iwapo dola milioni 101 hazitapatikana maramoja, wanafunzi 500,000 hawataweza kurudi shuleni mwezi huu.