Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Lishe ya maziwa yatumiwa kama ongezo katika matibabu ya HIV Tanzania

Lishe ya maziwa yatumiwa kama ongezo katika matibabu ya HIV Tanzania

Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na masuala ya ukimwi UNAIDS kupitia ripoti yake ya mapema mwaka huu linasema kwamba utafiti unaonyesha kwamba watu wakigundua hali yao ya HIV wanatafuta matibabu. Lakini matibabu yanapaswa kwenda sambamba na lishe bora, ili kuuwezesha mwili kupambana na kirusi cha HIV. Miongoni mwa vitu vilivyoonyesha kuwezesha mwili kuhimili makali ya HIV, ni maziwa. Je ni vipi maziwa yanatumika kama lishe? Basi ungana na Humphrey Mgonja wa Radio washirika Radio SAUTT kutoka Mwanza, Tanzania.