Skip to main content

Surua imeua watu 315 Katanga, DRC- OCHA

Surua imeua watu 315 Katanga, DRC- OCHA

Shirika la kuratibu masuala ya kibinadamu, OCHA, limesema kuwa mlipuko wa ugonjwa wa surua katika mkoa wa Katanga katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, umewaua watu 315 na kuwaambukiza wengine 20,000 tangu Januari mwaka huu.

Taarifa iliyotolewa leo na OCHA imesema mlipuko huo unaathiri wilaya 21 za afya kati ya wilaya 68.

Kumekuwa na visa 51,000 vya surua Katanga tangu mwaka 2012.

OCHA imesema pia kuwa milipuko ya surua hutokea sasa kila mwaka nchini DRC kwa sababu ya timu za kutoa chanjo kushindwa kuwafikia watu, kuhamahama kwa watu, uhaba wa dawa na imani za kienyeji na kijadi kuhusu chanjo.

Kwa mujibu wa OCHA, kati ya wilaya 21 zilizoathiriwa, ni saba tu ndizo zilizoweza kunufaika na kampeni za utioaji chanjo.