Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNAMID yakabidhi vifaa vya elimu kwa mamlaka ya Sudan, Darfur Magharibi

UNAMID yakabidhi vifaa vya elimu kwa mamlaka ya Sudan, Darfur Magharibi

Ujumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika huko Darfur, UNAMID umekamilisha kukabidhi kambi yake ndogo kwa serikali ya Sudan. Majengo hayo yalijengwa mwaka 2008 katika eneo ambalo lilitolewa na serikali ya Sudan, na yalitumika kama kituo rasmi cha wafanyakazi wa kiraia wa UNAMID na askari wake wakati ujumbe huo ukijenga ofisi zake.Taarifa kamili na Grace Kaneiya.

(Taarifa ya Grace)

Akihutubia umma wakati wa hafla hiyo, Afisa wa ngazi ya juu wa UNAMID  amemnukuu mkuu wake, Abidoun Bashua, akisema kwamba vifaa hiyvo vimekabidhiwa serikali ya Sudan kwa ajili ya kusaidia elimu ya vijana walioko Darfur Magharibi.

Taarifa ya UNAMD inasema kwamba majengo hayo yatatumika kutoa elimu katika chuo kikuu cha El Geneina. Kadhalika UNAMID imekanusha madai ya kwamba hili lilikuwa ni ombi kutoka kwa serikali huku ikisema kwamba imefanyika kwa hiari yake.

Akizungumzwa wakati wa hafla hiyo, Gavana wa Darfur Magharibi, Khalil Ali ameishukuru UNAMID na kusema kwamba vifaa hivyo vitatumika kwa njia nzuri na kwamba uharibifu kama wa awali wa vifaa kama hivyo vilivyotolewa na UNAMID hautafanyika chini ya uongozi wake.

Wakati huo huo serikali ya Japan imetoa msaada wa ofisi na vifaa vya kufundisha ikiwemo Kompyuta, viti na madawati kwa ajili ya chuo cha El Geneina.